Msanii wa muziki wa Bongo Fleva Dayna Nyange akikamua vilivyo usiku huu wa Valentine Day katika Ukumbi wa JB Belmonte Hotel katika jiji la Rocky City (Mwanza) ambapo katika ukumbi huo huo alikuwepo na mkali wa muziki Cindy Sanyu kutoka Nchini Uganda pamoja na wasanii wengine wa hapa jijini Mwanza.

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva Dayna Nyange akifanya mambo yake jukwaani usiku huu.

Dayna akiimba kwa hisia moja ya wimbo wake mbele ya mashabiki wake
Nivute kwako!!! ni wimbo wake msanii Dayna akiuimba vyema Jukwaani leo kwenye Ukumbi wa JB Belmonte Hotel katika jiji la Rocky City (Mwanza) leo Valentine Day.
Dayna Nyange amekamua nyimbo zake kadhaa huku wadau wakimkubali zaidi katika ukumbi huu. Cha zaidi kwa Dayna hakuweza kuficha tabasamu lake huku akijua ni sikukuu ya Wapendanao hivyo amekamua kisawasawa!!!
0 comments:
ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA
Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko PamojaPost a Comment