Mwananchi juu ya paa la nyumba ya mtu mmoja maarufu kwa jina la Mama Mayunga, akijaribu kurusha vifuko vya mchanga katika moja ya majengo ya nyumba iliyozuka moto Jana majira ya saa 5 asubuhi mtaa wa Majengo jirani na Masangwa Guest House wilayani Misungwi mkoani Mwanza.
Moto huo unaotajwa chanzo chake kusababishwa na jiko la gesi ulilipuka na kuiteketeza kabisa nyumba hiyo ikiwa na furniture zake.

Moto ukipamba moto na kutokea kwenye madirisha ukivuma.
Ingawa jeshi la polisi lilifika eneo la tukio na kuwasihi wananchi kusogea mbali toka eneo la moto kwani chanzo chake ni moto wa gesi katu watu hao hawakutii amri hiyo zaidi ya kuusogelea zaidi.

Hali ndiyo ilivyokuwa huku wananchi hao wa wilaya ya Misungwi wakisubiri huduma ya zimamoto toka magari ya Halmashauri ya jiji la Mwanza, umbali wa dakika 45.


.jpg)

0 comments:
ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA
Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko PamojaPost a Comment