Watoto hao wamefariki kwa mida tofauti
ambapo Mtoto wa Kwanza alifariki Nyumbani kwao baada ya kuugua ghafla ndipo
hali za wengine zilipoanza kutia shaka na kulazimu Waandishi wa Habari wa
Mtandao wa Mbeya Yetu, Gazeti la Jambo Leo na Redio ya Bomba Fm waliohudhuria
mazishi ya Mtoto huyo kulazimika kuwakimbiza katika Hospitali ya Wazazi Meta
kwa matibabu zaidi.
Hata hivyo baada ya kupokelewa kwa
watoto hao Watatu mtoto mmoja aliaga dunia baada ya kuchelewa kupata matibabu
kutokana na kubanwa na kifua na kusababisha kushindwa kupumua vizuri.
Hali za watoto wawili waliobaki
wanaendelea vizuri na matibabu na kwa mujibu wa Daktari anayewatibu amesema
taratibu za Hospitali hiyo ni kupokea watoto waliochini ya Miezi miwili lakini
hao wamezidi umri huo hivyo badala ya kupelekwa Hospitali ya Rufaa ya Mbeya
wataendelea kuwepo Meta hadi hapo hali zao zitakapoimarika.
Baadhi ya wananchi na wauguzi katika
Hospitali ya Wazazi Meta wamesema sababu ya watoto hao kuugua ni kutokana na
kukosekana kwa uangalifu wa karibu katika malezi ya watoto hao ukilinganisha
na maisha ya vijijini kukosa watu wenye uelewa wa afya za watoto.
Wengine wameitupia lawama moja kwa moja
Serikali kwa kushindwa kuchukua hatua za haraka tangu watoto walipozaliwa ili
kujiridhisha na mazingira wanayopaswa watoto hao kuishi kwa kuwapatia msaada wa
karibu na ushauri wa kitaalamu.
Kwa upande wake Afisa Ustawi wa Jamii Mkoa
wa Mbeya, Thobias Mwalwego, alikiri kuwepo kwa urasimu katika Idara yao kwa
madai kuwa tangu watoto hao walipokuwa wamezaliwa walipata taarifa na kuchukua
hatua kwa afisa mmoja kufika kijijini na kuchukua picha zao.
Alisema urasimu unakuja kutokana na
Ofisi ya Wilaya na Mkoa kukosa fungu la dharula ambapo barua za maombi zote
hupelekwa makao makuu kwa Kamishna wa Ustawi wa Jamii ambapo Ofisi yake
huchukua muda mrefu kurudisha majibu kutokana na waombaji kuwa wengi.
Alisema kila ofisi katika Ngazi ya Mkoa
ingekuwa na fungu la Dharula kama ilivyo katika Ofisi zingine hali ambayo
ingeweza kusaidia kuepusha vifo vya watoto hao kutokana na kupatiwa msaada wa
ushauri na makazi rafiki kwa malezi ya mapacha wanaozidi wawili.
Aidha alishauri kila Halmashauri Nchini
kutenga bajeti za kusaidia majanga kama hayo na vitu vya dharula wakati
Serikali inajipanga kutekeleza kutokana na taratibu zake kuchukua muda mrefu
ili kuweza kukabiliana na hali yoyote na muda muafaka.
CREDIT: Mbeya yetu.
Blogu hii inatoa pole kwa wazazi, ndugu,jamaa na wote walioguswa na misiba hii.
0 comments:
ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA
Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko PamojaPost a Comment