Kwa wale wadada waliokuwa wakisugua magoti kwa Mungu kupata kibali cha kuolewa na mwanakaka nyota wa kwaya ya Ambassadors of Christ ya Rwanda a.k.a Kwetu Pazuri Nelson Manzi ni wakati wa kubadirisha maombi yenu kuelekea kwa mtu mwingine maana mwanakaka amemuweka hadharani mkewe mtarajiwa kupitia ukurasa wake wa Facebook aitwaye Irakiza Eunice.
Nelson amejipatia umaarufu kokote kule ambako kanda za kwaya yake zinapatikana kutokana na uimbaji pamoja na tabasamu lake, mwanakaka huyu anaimba kwaya hiyo pamoja na dada yake kipenzi aitwaye Sarah Uwera ambaye ni mmoja wa masolo nyota wa kwaya hiyo kwasasa. GK inamtakia safari njema katika maisha ya uchumba hadi ndoa Mungu awatangulie.
Nelson Manzi akiwa na dada yake Sarah Uwera.©Nelson Manzi
CREDIT:gospelkitaa.co.tz
0 comments:
ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA
Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko PamojaPost a Comment