Wananchi Jimbo la Kiembesamaki, Zanzibar wakiangalia majina yao kujua vituo vyao walivyopangiwa kupiga kura leo asubuhi.
HABARI kutoka Zanzibar zinasema uchaguzi mdogo wa uwakilishi Jimbo la Kiembesamaki kisiwani humo unaendelea vizuri na wapiga kura wengi wamejitokeza kwenda kutimiza haki yao ya kimsingi.
Ulinzi umeimarishwa katika vituo vya kupigia kura.
Mwandishi wetu wa huko anasema jana kulikuwa na malumbano ya hapa na pale kwa wanachama wa vyama viwili vikubwa vya siasa, Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Chama Cha Wananchi (CUF), kwani walikuwa wakitambiana kila upande ukidai utashinda katika kinyang’anyiro cha leo.
Tutakuwa tukiendelea kuwapasha yanayotokea.
0 comments:
ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA
Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko PamojaPost a Comment